BREAKING NEWS: MAGUFULI AFUNGUA UKUTA WA MGODI WA TANZANITE, AFUNGUKA MAZITO.! - MR. KUYUMBO BLOG

Breaking

Friday, April 6, 2018

BREAKING NEWS: MAGUFULI AFUNGUA UKUTA WA MGODI WA TANZANITE, AFUNGUKA MAZITO.!


Leo Ijuma ya mwezi wa Tatu, Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefungua ukuta wa kuzunguka mgodi wa TANZANITE Mkoani Arusha ambao umejengwa kwa lengo la kuzuia sintofahamu zilizokuwa zikijitokeza awali.

Katika uzinduzi huo Rais Magufuli amezungumza mengi, ikiwemo suala la baadhi ya watu kufurahia nchi ikipata hasara "Watu ambao wanafurahia nchi ikiangamia ni sawa na mashetani" alisema Raisi Magufuli.

Magufuli ameahidi kushugulikia matatizo ya wachimbaji wadogowadogo na kusema kuwa atayatatua. Aidha amemwagiza waziri kukaa na wachimbaji hao ili kuona cha kufanya.

Katika hatua nyingine, Raisi Magufuli amemkabidhi Mkurugezi Funguo ya Gari aina ya Ambulance ili kusaidia katika shughuli mbalimbali.

No comments:

Post a Comment