BREAKING NEWS:SERIKALI KUWARUDISHA KAZINI WALIMU WA DARASA LA SABA NA WOTE WALIO FUKUZWA - MR. KUYUMBO BLOG

Breaking

Monday, April 9, 2018

BREAKING NEWS:SERIKALI KUWARUDISHA KAZINI WALIMU WA DARASA LA SABA NA WOTE WALIO FUKUZWA


Waziri, George Mkuchika, ameagiza watumishi wote ambao walikuwa na ajira za kudumu au ajira za mikataba (watendaji wavijiji na mitaa) au ajira za muda ambao walikuwa kazini kabla ya Mei 20, 2014 warejeshwe kazini na walipwe mishahara yao kwa kipindi chote.

Selikali pia imetangaza na kuwataka wakurugenzi kuwarudisha kazini walimu waliofukuzwa kazi kwa kigezo cha kuwa na elimu ndogo.

Walimu watakao rudishwa kazini ni wale ambao waliajiliwa kufikia Tarehe 20 may 2004. Hivyo zaidi ya walimu 1300 watarudishwa kazini.

Pia serikali imeongeza kuwa Walimu hao watatakiwa kulipwa fidia na mshahara wao wa tangu walipofukuzwa.

Kauli hii ya selikali imekuja siku chache baada ya bunge kutoa hoja hiyo bungeni ya kuitaka selikali kuwarudisha walimu waliofukuzwa kwa kutokuzingatia taratibu zote kurudishwa kazini.

No comments:

Post a Comment